Nyumbani » 08/11/2012 Entries posted on “Novemba 8th, 2012”

Katibu Mkuu ahuzunishwa na vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi Guatemala

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema umoja huo uko tayari kusaidi jitihada zinazofanywa na serikali ya Guatemala ya kutoa misaada ya kibinadamu kufuatia tetemeko la ardhi lililokumba nchi hiyo jana na kusababisha vifo vya watu 48 na wengine 150 kujeruhiwa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, msemaji wa Umoja wa [...]

08/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lashindwa kuridhia maazimio thabiti kuhusu Syria

Kusikiliza / Security Council Meeting:Non-proliferation

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kuridhia maazimio thabiti kuhuusu Syria, kwa mujibu wa katiba ya Umoja huo inayolipa baraza mamlaka ya kusimamia amani na utulivu duniani. Balozi wa Colombia katika Umoja wa Mataifa Néstor Osorio ametoa kauli hiyo wakati akitambulisha rasimu ya ripoti ya mwaka ya Baraza la Usalama itakayowasilishwa kwenye Baraza [...]

08/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwelekeo wa kuleta amani Libya unatia moyo: Mitri

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakifuatilia hotuba ya Tarek Mitri

Serikali ya Libya pamoja na wananchi wake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wamepiga hatua kubwa kurejesha utulivu nchini humo licha ya changamoto zilizopo. Hiyo ni kauli ya Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchiniLibya, Tarek Mitri aliyoitoa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wakati alipolihutubia kuhusu hali ilivyo nchini Libya [...]

08/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fedha zaidi zahitajika kusaidia chakula na watoto waende shule nchini Mali: OCHA

Kusikiliza / malipopulation

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA limesema hali ya kibinadamu nchini Mali si nzuri na kwamba watu Milioni Nne nukta Sita nchini humo bado hawana uhakika wa chakula. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nesirky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani kuwa uwezo wa wakazi wa kaskazini mwa [...]

08/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yatoa mafunzo kusaidia uandaaji wa vipindi bora kuhusu Ukimwi

Kusikiliza / washiriki katika komgamano la UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO linaendesha mafunzo ya siku tano kwa waandaji wa vipindi vya radio wa nchi za Afrika Mashariki kwa ajili ya kuongeza ubora wa vipindi vya elimu kuhusu kinga dhidi ya Ukimwi na kuimarisha ushirikiano baina ya Radio katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika mafunzo hayo [...]

08/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa dawa za kuzuia kichocho nchini Nigeria

Kusikiliza / Nembo ya WHO

  Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa zaidi ya tembe milioni tano za kuuwa minyoo inayosababisha ugonjwa wa kichocho kwa serikali ya Nigeria, ili kusaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo unaoainishwa miongoni mwa magonjwa ya kitropikali yalosahaulika. Idadi ya watu watakaolindwa kutokana na ugonjwa huo inakadiriwa kuwa milioni tatu. Ugonjwa wa kichocho huzuia ukuaji wa [...]

08/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa kipalestina watendewe haki: Kamishna Mkuu UNRWA

Kusikiliza / Fillipo Grandi

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada na ulinzi wa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA Fillipo Grandi ametaka suluhisho la haki kwa zaidi ya wakimbizi Milioni Tano wa kipalestina. Akiwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Grandi ameelezea pia wasiwasi wake mkubwa kwa hali [...]

08/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kongamano la udhibiti wa Intaneti lasisitizia usalama wa wanaharakati wa tovuti za Intaneti

Kusikiliza / IGF

Uhuru wa kuwa na usemi kupitia kwa njia ya Intaneti umepata uungwaji mkono wa dhati katika kongamano la Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuhusu udhibiti wa mfumo wa Intaneti mjini Baku, Azerbaijan. Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi wa kitengo cha uhuru wa kuwa na usemi na maendeleo ya vyombo vya habari, Guy Berger, [...]

08/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNRWA yaeleza wasiwasi juu mashambulio dhidi ya wakimbizi wa kipalestina

Kusikiliza / nembo ya UNRWA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada na ulinzi kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA imezieleza mamlaka ya Syria juu ya hofu yake kuu kwa madhara wanayopata wakimbizi wa kipalestina kutokana na mgogoro unaoendelea nchini humo. Hofu hiyo inafuatia mauaji ya Jumatatu ya Dkt. Rehab Awadallah, mwalimu wa UNRWA nchini Syria pamoja na mpwa wake [...]

08/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za ASEAN ziangalie upya rasimu ya azimio lake kuhusu haki za binadamu: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

  Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay amesifu kongamano la Bali kama fursa muhimu ya kuendeleza utawala bora, utawala wa kisheria na haki za binadamu miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Kusini- Mashariki mwa Asia, ASEAN huku akitaka viongozi wa nchi hizo kuweka muda [...]

08/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bei ya chakula ilishuka kidogo mwezi Oktoba: FAO

Kusikiliza / food 2

Bei ya chakula ilishuka kwa asilimia moja ya kipimo wastani cha Shirika la Chakula na Kilimo, FAO mnamo mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha katika kipindi cha miezi kumi ya kwanza mwaka huu, bei ya chakula ilikuwa asilimia 8 wastani, na hivyo kuwa chini ya ilivyokuwa katika kipindi sawa na hicho mwaka 2011. Bei ya kapu [...]

08/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Sudan iharakishe uchunguzi wa ripoti za shambulio huko Sigili: UNAMID

Kusikiliza / unamid darfur

Kaimu Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID, Aichatou Mindaoudou ametaka serikali ya Sudan kuharakisha mchakato wa uchunguzi wa ghasia zinazoripotiwa kutokea kijiji cha Sigili. Ametoa agizo hilo kufuatia ripoti za hivi karibuni zinazodai kuwepo kwa shambulio dhidi ya raia siku ya Ijumaa kwenye kijiji cha [...]

08/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031