Nyumbani » 07/11/2012 Entries posted on “Novemba 7th, 2012”

Jumuiya ya kimataifa isaidie Libya kukabiliana na ukwepaji wa sheria: Bensouda

Kusikiliza / Fatou Bensouda

Mwendesha Mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, Fatou Bensouda ameitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia Libya kuondoka na vitendo vya kukwepa kuchukua mkono wa sheria na badala yake kusimamia utawala wa kisheria. Bi.Bensouda amesema hayo leo mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati akiwasilisha ripoti yake ambapo ameeleza kuwa [...]

07/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yashukuru Lebanon kwa kusaidia wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Ertharin Cousin

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin, amehitimisha ziara yake nchini Lebanon na kuipongeza serikali ya nchi hiyo na wananchi wake kwa kuwasaidia wakimbizi kutoka Syria wanaotafuta hifadhi salama. Bi. Cousin ambaye amewaeleza waandishi wa habari mjini Beirut kuwa kitendo hicho cha serikali ya Lebanon kinarahisisha kazi ya WFP ya [...]

07/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasaidia kusuluhisha matatizo ya ardhi kaskazini mwa Sri Lanka

Kusikiliza / tizo ya ardhi, Sri lanka

Miaka mitatu tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka, changamoto mpya zimeibuka wakati watu wakiendelea kurejea nyumbani. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limekuwa likishirikiana na viongozi wa kitaifa na wadau wengine ili kusaidia kuhakikisha wakimbizi hao wanarejea kwa njia endelevu kwa kuzishughulikia baadhi ya changamoto hizo, zikiwemo [...]

07/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaipongeza Philippines kwa kuanzisha mpango unaowajali wakimbizi

Kusikiliza / wakimbizi wa Ufilipino

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limepongeza serikali ya Philippines kwa kuwa nchi ya kwanza katika eneo la Asia-Pasifik kuanzisha mpango wenye shabaha ya kuwalinda wakimbizi na jamii ya watu wasiokuwa na ukazi maalumu. Idara ya haki na sheria ya Philipenes hivi karibuni ilichapisha mwongozo ambao pamoja na mambo mengine umekusudia kuboresha [...]

07/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

AMISOM yaongezewa miezi minne zaidi nchini Somalia

Kusikiliza / AMISOM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza kwa miezi minne zaidi muda wa kuwepo nchini Somalia kwa vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini humo, AMISOM. Uamuzi huo umeazimiwa leo wakati wa kikao cha baraza hilo mjini New York Marekani ambapo muda wa awali wa wiki moja ulioongezwa wiki iliyopita ulikuwa unamalizika leo. Rais [...]

07/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utafiti mpya wa UNCTAD wazingatia sera za kibiashara na usawa wa kijinsia katika nchi tatu

Kusikiliza / nembo ya UNCTAD

Sera za kibiashara huathiri kwa njia tofauti sehemu mbali mbali za jamii, kama vile wanaume na wanawake, wakaazi wa vijijini na mijini, watu tajiri na maskini. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo, UNCTAD, wa hali katika nchi za Cape Verde, the Gambia na Lesotho. [...]

07/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO na Pakistani waandaa tukio maalum kutetea elimu kwa mtoto wa kike

unesco-logo

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova na Rais Asif Al Zardani wa Pakistani watakuwa wenyeji wa tukio mkutano maalum wa ngazi ya juu wa kutetea haki ya elimu kwa mtoto wa kike. UNESCO imesema mkutano huo ukiwa na maudhui, Mtetee Malala, tetea hali mtoto wa [...]

07/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Katiba mpya na maoni ya umma zinatoa nafasi nzuri kwa Kenya kulinda misitu yake: UNEP

Kusikiliza / misitu

Kenya inafaa kuidakia fursa maalum ilotolewa na katiba yake mpya, pamoja na maoni ya umma ili kukomesha uharibifu wa misitu katika maeneo yake ya maji, ambao husababisha hasara ya dola milioni sabini kila mwaka kwa uchumi wake, na kuweka hatarini asilimia sabini ya vianzo vya maji nchini humo. Hayo ni kwa mujibu wa wajumbe waliohudhuria [...]

07/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Homa ya manjano yazidi kusambaa jimbo la Darfur: WHO

Kusikiliza / homa ya manjano

Shirika la afya duniani, WHO limesema idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa homa ya manjano kwenye jimbo la Darfur, huko Sudan imefikia 67 huku idadi ya wagonjwa ikiongezeka maradufu kutoka 84 wakati ugonjwa huo uliporipotiwa hadi 194. Kwa mara ya kwanza ugonjwa huo unaoenezwa na mbu, uliripotiwa mwezi Oktoba na umeshaenea katika vitongoji 17 [...]

07/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ampongeza Obama kwa kuchaguliwa tena kuongoza Marekani

Kusikiliza / Rais Barack Obama na KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amemtumia salamu za pongezi kwa Rais Barack Obama wa Marekani kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka minne na kusema ni matarajio yake kuendelea kufanya kazi na Rais Obama na serikali yake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa. [...]

07/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko yaanza kupungua taratibu Nigeria: OCHA

Kusikiliza / Mafuriko Nigeria

Mafuriko yaliyokumba Nigeria kutokana na mvua zilizonyesha kati ya mwezi Julai na Oktoba mwaka huu yameanza kupungua wakati huu ambapo mamlaka ya hali ya hewa nchini huumo imetangaza kuwepo kwa mvua zaidi mwezi ujao zenye uwezekano mdogo wa kuleta madhara. Ripoti ya awali ya hali halisi ya mafuriko nchini Nigeria iliyotolewa na shirika la Umoja [...]

07/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031