Nyumbani » 06/11/2012 Entries posted on “Novemba 6th, 2012”

UM waanza kusambaza chakula kwenye jimbo la Rakhine, Myanmar

Kusikiliza / myanmar-family-idp-camp1

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limeanza kusambaza chakula kwa zaidi ya wakazi Elfu 27 wa vitongoji vilivyokumbwa na mgogoro wa kikabila kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar mwezi uliopita.   Msemaji wa WFP Elisabeth Byrs amewaeleza waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa idadi hiyo ya wat wanaopatiwa msaada ambao [...]

06/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Taka ni tatizo linahatarisha usafi wa maji, hewa, chakula duniani na afya: UNEP

Kusikiliza / taka

Takriban tani bilioni 1.3 za taka huzalishwa mijini kila mwaka, na kiwango hiki kinatarajiwa kuongezeka hadi tani bilioni 2.2 ifikapo mwaka 2025, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia. Kwa sababu hii, hatua za haraka zinahitajika ili kukabiliana na athari za tatizo hili kwa maisha ya mwanadamu, limesema Shirika la Mpango wa Mazingira la [...]

06/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhuru wa kujieleza ndio kiungo muhimu cha kumaliza lugha za chuki:UM

Kusikiliza / Frank La Rue

Uhuru wa kujieleza unaweza kuchangia kuwepo kwa mazingira bora ya kuwepo kwa mazungumzo ya kukosoana hasa katika masuala ya kidini amesema mtalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza Frank La Rue. Kupitia kwa ripoti yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjumbe huyo amezungumzia masuala ya lugha inayozua chuki na hatua za [...]

06/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Haiti yahitaji mamilioni ya fedha kwa ajili ya sekta ya kilimo iliyoharibiwa na Sandy: FAO

Kusikiliza / mafuriko nchini Haiti

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na serikali ya HAITI zinahitaji zaidi ya dola Milioni 74 katika kipindi cha miezi 12 ijayo kwa ajili ya kurekebisha sekta ya kilimo nchini humo iliyoharibiwa na kimbunga Sandy. Kimbunga hicho kilichopiga mwishoni mwa mwezi uliopita kimeharibu miundombinu maeneo ya vijijini pamoja na mazao, ardhi, mifugo, mashamba ya [...]

06/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa WHO kuhusu matumizi ya tumbaku kufanyika Seoul, Korea Kusini

Kusikiliza / matumizi ya tumbaku

Mkutano wa Shirika la Afya Duniani kuhusu mkataba wa kudhibiti bidhaa za tumbaku unatazamiwa kufanyika mjini Seoul, Korea Kusini wiki ijayo, ukiwa ni mkutano wa tano wa mataifa wanachama wa mkataba huo. Mkutano huo wa wanachama unatazamiwa kurejelea, kufanyia marekebisho na kuendeleza utekelezaji wa mkataba huo. Inatarajiwa kuwa mwishoni mwa mkutano huo, mkakati wa kwanza [...]

06/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa dharura wa chakula unatakiwa Haiti: WFP

Kusikiliza / WFP, Haiti

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema linahitaji dola Milioni 20 kwa ajili ya msaada wa chakula kwa watu Laki Mbili na Elfu Ishirini na Tano nchini Haiti wanaokabiliwa na matatizo kutokana na kimbunga Sandy kilichokumba nchi hiyo. Msemaji wa WFP Elizabeth Byrs amesema hivi sasa watu hao wamepoteza makazi yao, mazao na kwamba [...]

06/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makao makuu ya idara ya uhamiaji yafunguliwa Somaliland

Kusikiliza / nembo ya IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua makao makuu mapya ya idara ya uhamiaji katika mji mkuu wa Somaliland Hargeisa. Mradi huu unatarajiwa kuwezesha idara ya uhamiaji eneo la Somaliland kutoa usimamizi wa mipaka unaohitajika. Uzinduzi wa makao hayo ulihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini wakiongozwa na rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Mohamoud [...]

06/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Raia wa Sudan Kusini walioko Khartoum waanza kurejeshwa Aweil: IOM

Kusikiliza / raia wa Sudan Kusini warejea nyumbani kwa ndege

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali za Sudan na Sudan Kusini zimeanza kusafirisha raia Elfu Moja Mia Tatu Sabini wa Sudan Kusini kutoka mji mkuu wa Sudan, Kharthoum kwenda mji wa Aweil ulioko jimbo la Bahr El Ghazal, Sudan Kusini. Raia hao pamoja na familia zao ni wale walioko katika mazingira magumu zaidi na [...]

06/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maliasili zitumike kuleta amani na si migogoro: Ban

Kusikiliza / maliasili

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ametaka hatua zaidi zichukuliwe kuepusha migogoro katika nchi inayochochewa na kuwepo kwa maliasili na badala yake utajiri huo utumike vyema kujenga amani. Bwana Ban amesema hayo leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuepusha mizozo itokanayo na matumizi mabaya ya maliasili ambapo ameongeza kuwa laana ya kumiliki [...]

06/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031