Nyumbani » 05/11/2012 Entries posted on “Novemba 5th, 2012”

Baraza la Usalama libadili makubaliano kuwa azimio ili kumaliza mzozo Syria: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdir Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu, Lakhdar Brahimi amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa libadilishe kuwa azimio, makubaliano ya mwezi Juni kuhusu hatua za kuweka kipindi cha mpito nchini Syria kwa lengo la kusaidia kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo. Brahimi amesema hayo leo huko Cairo, [...]

05/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nishati ya nyuklia bado ni muhimu kukidhi mahitaji ya nchi: India

Kusikiliza / IAEA

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limeelezwa kuwa nishati ya nyuklia bado ni mbadala muhimu wa kukidhi mahitaji ya nishati duniani licha ya ajali iliyokumba mtambo wa nyuklia wa Fukushima Daiichi nchini Japan mwaka jana. Afisa wa India kwenye Ubalozi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa Annu Tandon ametoa kauli hiyo wakati baraza [...]

05/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu nchini DRC ni mbaya: OCHA

Kusikiliza / John Ging

Mkurugenzi wa Operesheni wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa, OCHA. John Ging amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani na kusema kuwa hali ya kibinadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC ni mbaya wakati huu ambapo zaidi ya watu Milioni Mbili wamekimbia makazi yao ndani ya nchi [...]

05/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wahoji hatua ya serikali ya Sudan Kusini kumfukuza afisa wake wa haki za binadamu

Kusikiliza / Hilde Johnson

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, Hilde Johnson, amesema hatua ya serikali ya Sudan Kusini kumfukuza afisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ni kinyume na wajibu wa serikali hiyo chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini iliiandikia afisi ya ujumbe wa Umoja wa [...]

05/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Asia Pasifiki zaridhia mpango wa kujenga jamii inayojumuisha walemavu

Kusikiliza / mpango wa maridhiano

Mataifa 39 ya Asia-Pasifiki yameridhia kuanzisha muundo wenye lengo la kujenga jamii inayojumuisha watu wenye ulemavu kwenye ukanda huo wenye walemavu zaidi ya Milioni 650. Makubaliano hayo yanayoitwa mkakati wa muongo mmoja wa Incheon yamefikiwa mwishoni mwa mkutano wa aina yake wa masuala ya Umoja wa mataifa kwenye ukanda huo huko Korea Kusini ambapo ulitathmini [...]

05/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Haiti yaomba msaada wa UM baada ya Kimbunga Sandy

Kusikiliza / kimbunga-sandy

Umoja wa Mataifa umesema kuwa yapata watu milioni 1.6 nchini Haiti wameathirika vibaya sana na kimbunga Sandy, ambacho kilipita pwani ya mashariki mwa Marekani na maeneo ya Karibi wiki moja iliyopita. Serikali ya Haiti imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na wafadhili kutoa misaada ya dharura ili kuwasaidia manusura na waathirika wa [...]

05/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tathmini ya mkataba wa kimataifa wa urithi wa dunia kufanyika Kyoto: UNESCO

Kusikiliza / urithi wa dunia, Kyoto-Japan

Mkutano wa siku Tatu wa kuhitimisha kilele cha maadhimisho yaa miaka 40 ya mkataba wa kimataifa wa urithi wa dunia utafanyika mjini Kyoto Japan kuanzia kesho ambapo pamoja na mambo mengine utajumuisha mijadala kuhusu utekelezaji wa mkataba huo. Tukio hilo linatarajiwa kushuhudia kuingizwa kwa eneo la 1000 la urithi wa dunia kwa mujibu wa mkataba [...]

05/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sekta ya Viwanda yataka mfumo wa UNFC utumike kwa vyanzo asilia vya nishati

Kusikiliza / vyanzo asilia vya nishati

Watalaamu kuhusu nishati asilia wamesema kuna umuhimu wa kuwa na mfumo mmoja na wa uwazi zaidi wa kutathmini na kufahamu idadi ya vyanzo asilia vya nishati kwa uwazi wakati huu ambapo sekta hiyo na nishati asilia inakuwa ya kibiashara zaidi. Jopo la wataalamu hao lilikuwa na mkutano huko London, Uingereza kwa siku tatu kuanzia tarehe [...]

05/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukataji wa miti waigharimu Kenya mamilioni ya dola kila mwaka: UNEP

Kusikiliza / ukataji miti, Kenya

Kenya ilipoteza jumla ya shilingi bilioni 5.8 au dola milioni 68 mwaka 2010 na shilingi bilioni 6.6 mwaka 2009 kutokana na ukataji wa miti kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na idara ya misitu nnchini Kenya KFS. Utafiti unoaendeshwa na na idara ya misitu nchini Kenya [...]

05/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia zaendelea kuwalazimu watu zaidi kuhama nchini Myanmar

Kusikiliza / myanmar-family-idp-camp1

Idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao kutokana na ghasia za kisiasa kwenye mkoa wa Rakhine nchini Myanmar imefikia watu 110,000 kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA. Takriban watu 89 wameuawa tangu kuanza kwa kwa mzozo mwezi Oktoba huku zaidi ya nyumba 5,300 na maeneo ya kuabudu vikiharibiwa. [...]

05/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930