Nyumbani » 02/11/2012 Entries posted on “Novemba 2nd, 2012”

AMISOM yaongezewa wiki moja zaidi nchini Somalia

Kusikiliza / Askari wa kulinda amani nchini Somalia

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza kwa siku saba zaidi muda wa kuwepo kwa vikosi vya kimataifa vinavyolinda amani nchiniSomalia.  Muda wa vikosi hivyo ulikuwa umalizike tarehe 31 mwezi uliopita. Taarifa iliyotolewa imesema kuwa azimio la Barazahilolililopitishwa kwa kauli moja mjiniNew York, Marekani baada ya kikao chake, limeongezwa muda huo kwa kuzingatia mazingira [...]

02/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya uchunguzi dhidi ya ugaidi ipewe mamlaka zaidi: Emmerson

Kusikiliza / Baraza Kuu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na utetezi wa haki za binadamu na uhuru wa kujieleza wakati wa harakati zozote za kupinga ugaidi, Ben Emmerson amelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo kuhakikisha vikwazo vyake dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Al Qaeda vinazingatia haki za binadamu. Emmerson amesema hayo leo mbele ya Baraza [...]

02/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Majaji wa ICC waamua Laurent Gbagbo ana afya ya kukabili mashtaka

Kusikiliza / Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo

Jopo la majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Kivita, ICC, limeamua leo Novemba 2 kuwa aliyekuwa rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo yu bukheri wa afya na hivyo anaweza kusimama mashtaka mbele ya mahakama hiyo. Majaji hao wataweka tarehe karibuni ya kusikiliza kuthibitishwa kwa mashtaka katika kesi dhidi ya Bwana Gbagbo. Kwa mujibu wa uamuzi [...]

02/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yakabiliwa na uhaba wa fedha kuwasaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

Kusikiliza / mafuriko, Pakistan

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limeshindwa kuendesha juhudi za kuwakwamia mamia ya raia wa Pakistan waliokumbwa na mafuriko kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha. Takwimu kutoka serikali zinasema kuwa kiasi cha watu milioni 3.4 wameathiriwa na mafuriko huku wengine zaidi ya 386,000 hawana makazi maalumu kutokana na nyumba zao kubomolewa [...]

02/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa mashine za kupumulia wasababisha vifo vya watoto Syria: UNICEF

Watoto nchini Syria

Umoja wa Mataifa umesema idadi kubwa ya watoto wachanga nchini Syria wanafariki dunia kutokana na uhaba wa mashine za kuwawezesha kupumua pindi wanapozaliwa kabla ya wakati. Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema jopo la wataalamu wake lilitembelea jimbo la Al Raqqah nchini Syria ambapo hospitali kuu ya eneo hilo ina mashine [...]

02/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasema misaada ya chakula na malazi yahitajika haraka Rakhine

Kusikiliza / mafuriko, Rakhine

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema wafanyakazi wake wameweza kufika katika vijiji vilivyokumbwa na mapigano kwenye jimbo la Rakhine, magharibi mwa Myanmar ambako serikali ya nchi hiyo imesema watu 35, 000 wamepoteza makazi kutokana na vurugu hizo za hivi karibuni. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards, amesema ziara ya wafanyakazi hao inafuatia [...]

02/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misukosuko yasababisha kuhama kwa watu zaidi nchini DRC

Kusikiliza / wakimbizi DRC

Kuendelea kuwepo kwa misukosuko kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kumechangia kuongozeka kwa idadi ya watu wanaohama makwao nayo mahitaji ya chakula yakizidi kupanda. Zaidi ya watu 260,000 wamalazimika kuhama makwao kwenye mkoa wa Kivu kaskazini tangu kuanza kwa mzozo mwezi Aprili mwaka huu. Juma hili shirika la mpango wa [...]

02/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna wakimbizi zaidi wa ndani nchini Mali: UNHCR

Kusikiliza / Mali

Takwimu kutoka nchini Mali zinaonyesha kuwa kuna idadi ya juu ya wakimbizi wa ndani nchini kuliko ilivyoripotiwa awali.Kulingana na tume unayohusika na kuhama kwa watu nchini Mali nchini ya uongozi wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ni kwamba watu 203,845 wamelazimika kuhama makwao. Pia kumekuwa na dalili za watu kuhama ambapo [...]

02/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kutoa misaada yakabiliana na athari za kimbunga Sandy nchini Haiti

Kusikiliza / ugonjwa wa kipindupindu, Haiti

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa kimbunga Sandy kinaripotiwa kuwaua watu 60 nchini Haiti na kuwaathiri wengine milioni 1.8 ambapo pia nyumba 18,000 ziliharibiwa. Kwa upande wake shirika la afya duniani WHO linasema kuwa hali mbaya ya usafi nchini Haiti huenda ikachangia kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza ukiwemo [...]

02/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya Syria kwenye video huenda yakawa uhalifu wa kivita: OHCHR

Kusikiliza / Rupert Colville

Mauaji ya wanajeshi wa serikali ya Syria kwa kufyatuliwa risasi na vikosi vya upinzani, na ambayo yalinaswa kwenye video, huenda yakaainishwa kama uhalifu wa vita, kwa mujibu wa afisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadam katika Umoja wa Mataifa. Afisi hiyo ya haki za binadam imetoa wito kwa pande zote katika mzozo wa Syria [...]

02/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu Bilioni 2.2 wako hatarini kukumbwa na Malaria huko Asia–Pasifiki

Kusikiliza / mbu wa kuambukiza malaria

Zaidi ya watu Bilioni 2.2 katika nchi za Asia-Pasifiki wako hatarini kukumbwa na ugonjwa wa Malaria, ugonjwa ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukitajwa kuwa tishio barani Afrika pekee. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya mpango wa ushirikiano wa kimataifa wa kudhibiti Malaria, RBM ambayo imesema nchi za India, Myanmar, Papua New Guinea [...]

02/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya wakimbizi wa kipalestina Syria yakomeshwe: UNRWA

Kusikiliza / wakimbizi wa kipalestina

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada kwa ajili ya wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limeendelea kuonyesha wasiwasi wake juu ya madhara ya mgogoro wa Syria kwa wakimbizi wa kipalestina na raia wa nchi zingine na hivyo kutaka pande zote katika mgogoro huo kujizuia kufanya mashambulizi ya kiholela kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Wito [...]

02/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Akili nchini Burundi

Kusikiliza / ugonjwa wa akili

Watalamu wa kimatibabu wanasema magonjwa ya akili ni moja wapo wa maradhi yanayopuuzwa sana, hasa katika nchi zinazoendelea. Asilimia sabini na tano ya watu wanaokumbwa na magonjwa ya akili wanaishi katika nchi zinazoendelea na wengi wao hawapati matibabu. Mara nyingi, usumbufu wa akili huwapunguzia watu uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha za kila siku, [...]

02/11/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu yazidi kudorora Syria wakati msimu wa baridi kali ukikaribia

Kusikiliza / hali ya kibinadamu yazidi kudorora, Syria

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema kadri mzozo unavyozidi kuimarika nchini Syria, hali ya kibinadamu inazidi kudorora wakati huu ambapo idadi ya wanaohitaji misaada ya kibinadamu nchini humo ikiongezeka na kufikia watu Milioni Mbili na Nusu. Jarida la hali ya kibinadamu linalotolewa na OCHA limesema misaada ya kibinadamu wakati wa [...]

02/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wataka China kushughulikia masuala ya haki za binadamu huko Tibet

Kusikiliza / Navi Pillay

Umoja wa Mataifa umeitaka China kushughulikia haraka iwezekanavyo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyochochea maandamano na vurugu huko Tibet ikiwemo watu kujiua kwa kujichoma moto. Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema tangu mwaka 2011 kumekuwepo na matukio zaidi ya 60 ya watu kujiua kwa kujichoma [...]

02/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031