Nyumbani » 01/11/2012 Entries posted on “Novemba 1st, 2012”

UM yapongeza kuundwa kwa serikali mpya nchini Libya na kusisitiza mashauriano

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Libya, Tarek Mitri.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Tarek Mitri amempongeza Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan na baraza lake la mawaziri kufuatia kuundwa kwa serikali mpya nchini humo. Mitri, katika taarifa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia Libya, UNSMIL amelipongeza pia bunge la Libya kwa kuidhinisha serikali hiyo na [...]

01/11/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tathmini ya uharibifu nchini Haiti kutokana na kimbunga inafanyiwa majumuisho: OCHA

Kusikiliza / Wananchi wa Haiti wakipatiwa msaada

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA nchiniHaiti, Johan Peleman amesema wanasubiri ripoti ya majumuisho ya tathmini ya madhara yaliyotokana na kimbungaSandykilichopiga nchi hiyo wiki iliyopita ili waweze kufahamu msaada unaohitajika na idadi kamili ya watu walioathiriwa wakati huu ambapo inakadiriwa watu Elfu Ishirini hawana makazi. Peleman ameiambia Radio [...]

01/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM ataka mashauriano kati ya serikali na vyama vya kijamii Belarus

Kusikiliza / Miklós Haraszti

Mtaalamu mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchiniBelarus, Miklós Haraszti ametaka kufanyika kwa mjadala wa wazi kati yake na serikali ya nchi hiyo pamoja na vyama vya kijamii wenye lengo la kuendeleza na kulinda haki za binadamu nchini humo. Haraszti amesema hayo leo ikiwa ni siku anayoanza rasmi jukumu hilo alilokabidhiwa na [...]

01/11/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM waitaka Iran iwaachilie huru washindi wa Tuzo ya Sakharov mara moja

Kusikiliza / tuzo ya SAKHAROV

Jopo la wataalam huru wa Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa serikali ya Iran iwaachilie huru mara moja wakili maarufu wa kutetea haki za binadamu, Nasrin Sotoudeh na Jafar Panahi, ambaye ni mtengenezaji filamu mwenye umaarufu wa kimataifa. Wawili hao walipewa tuzo ya uhuru wa dhana ya Sakharov hivi karibuni na bunge la Jumuiya ya [...]

01/11/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jitihada za kusambaza misaada Syria zilifanikiwa kwa kiasi licha ya changamoto: UNHCR

Kusikiliza / UNHCR yatoa msaada kwa watu wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema wakati wa sikukuu ya Eid El Adha lilifanikiwa kwa kiasi fulani kuwasilisha misaada ya kibinadamu kwa baadhi ya maelfu ya familia nchini Syria ambazo awali zilikuwa haziwezi kupatiwa misaada hiyo. Msemaji wa UNHCR Ron Redmond amesema ghasia ziliendelea kwa kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano hayakuzingatiwa [...]

01/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wachunguza usafirishaji haramu wa binadamu Ufilipino

Kusikiliza / Biashara ya watu

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limemtuma mtaalamu huru kuhusu masuala ya usafirishaji haramu wa binadamu kwenda nchini Ufilipino kuchunguza hali halisi usafirishaji haramu wa binadamu nchini humo na athari za mikakati ya kupambana na vitendo hivyo. Mtaalamu huyo Joy Ngozi Ezielo ataanza ziara hiyo tarehe Tano mwezi huu hadi tarehe Tisa [...]

01/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yataka mauaji ya waandishi wa habari Somalia yachunguzwe

Kusikiliza / vyombo vya waandishi habari

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, ameelezea kusikitishwa kwake kuhusu usalama wa waandishi habari nchini Somalia, na kutaka uchunguzi ufanywe kufuatia mauaji ya Mohammed Mohamud Tuuryare na Ahmed Farah Ilyas mnamo Oktoba 28 na Oktoba 23 mfululizo. Bi Bokova amelaani mauaji hayo, na kusema kuwa idadi ya waandishi habari [...]

01/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Homa ya Marburg yaendelea kusambaa nchini Uganda

Kusikiliza / marburg

Shirika la afya duniani, WHO limesema ugonjwa wa homa ya Marburg umeendelea kusambaa nchini Uganda ambapo hadi sasa watu Kumi na Mmoja wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Wagonjwa 20 wameripotiwa katika wilaya Tano nchini humo ikiwemo kwenye mji mkuu Kampala. Homa ya Marburg iliripotiwa kulipuka katika wilaya ya Kabale Kusini Magharibi mwa Uganda tarehe [...]

01/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kutokomeza polio haziwafikii walio hatarini zaidi: WHO

Kusikiliza / polio-pakistan

Ugonjwa wa kupooza, yaani polio, hautatokomezwa nchini Pakistan pasi mpango wa kitaifa kuwafikia wazazi kutoka makundi ya jamii ambayo yamo hatarini zaidi, kama vile jamii za kipato cha chini za Pashtun, ambazo huathiriwa zaidi na ugonjwa huo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyochapishwa kwenye taarifa ya habari ya Shirika la Afya Duniani, [...]

01/11/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930