Zaidi ya wakimbizi 25,000 kutoka DRC warudi makwao kutoka nchini Congo

Kusikiliza /

wakimbizi wa RDC

Shirika la UNHCR limesema kuwa limewasaidia zaidi ya raia 25,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kurudi makwao kaskazini mwa nchi kutoka nchi jirani ya Congo kupitia mpango wa kuwarejesha nyumbani kwa hiari uliozinduliwa mwezi Mei. UNHCR inasema inamatumaini ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi 24,000 wengi kutoka mkoa wa Equateur ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na 32,000 zaidi mwaka ujao.

Hadi sasa kuna zaidi ya wakimbizi 100,000 kutoka DRC walio nchini Congo. Wakimbizi hao wamekuwa wakiishi kwenye maeneo yaliyotengwa kando kando mwa mto Oubangui baada ya kukimbia mapigano ya kikabila kwenye mkoa wa Equateur mwaka 2009. Edrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031