WHO yalaani mashambulizi katika vituo vya afya nchini Syria

Kusikiliza /

mhudumu wa afya, Syria

Shirika la afya duniani, WHO limelaani vikali kitendo cha mashambulizi katika vituo vya afya nchini Syria na kueleza wasiwasi wake juu ya madhara ya mashambulizi hayo kwa wahudumu wa afya, wagonjwa na miundombinu ya afya.

Taarifa ya WHO imesema kuwa mpaka sasa asilimia 67 ya hospitali za umma nchini humo zimeathiriwa na mgogoro huo na kati ya hizo asilimia 29 haziwezi kutoa huduma kabisa huku magari ya kubebea wagonjwa yakiharibiwa au kutumiwa isivyopaswa na hivyo kukwamisha usafirishaji wa wagonjwa.

Kwa mantiki hiyo, WHO imekumbusha wajibu wa pande zote husika kwenye mgogoro huo wa kulinda raia, vituo na wahudumu wa afya kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kulinda binadamu ambapo vituo vya afya havipaswi kuhusishwa na migogoro.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031