WHO yaangazia umuhimu wa kujitambulisha kwenye siku ya afya ya akili duniani

Kusikiliza /

siku ya afya ya akili

Mojawepo pingamizi katika kutibu matatizo ya akili ni kwamba watu huwa hawajitambulishi na kutafuta msaada. Kauli hiyo imetolewa na Dr. Shekar Saxena kutoka Shirika la Afya Duniani, WHO, katika kuadhimisha siku ya afya ya akili duniani, leo tarehe kumi Oktoba.

Dr. Saxena, ambaye ni mkurugenzi wa afya ya akili na matumizi mabaya ya dawa, amesema usumbufu wa akili ni ugonjwa ambao humfanya mtu akiwa amehuzunika kwa kwa muda wa wiki mbili au zaidi, na ambao huathiri utendaji kazi na maisha ya kila siku.

Dr. Saxena akitoa mfano wa wabunge wawili kutoka bunge la Uingereza, Dr. Saxena amesema watu wakijitambulisha kuwa wana usumbufu wa akili, wanaweza kusaidiwa na kurejelea maisha yao ya kawaida.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031