WFP yatoa msaada kwa watu wanaokumbwa na uhaba wa chakula Yemen

Kusikiliza /

uhaba wa chakula, Yemen

Baada ya hali ya kibinadamu kuendelea kuwa mbaya nchini Yemen shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekuwa likipanua programu za kusaidia wanaotaabika. Mwanzo wa mwaka huu WFP ilipanga kusambaza misaada kwa watu milioni 1.2 . Mwezi Mei idadi hiyo ikaongezeka hadi watu milioni 1.8. Mwezi Septemba ikaongeza tena kwa watu milioni mbili hadi watu milioni 3.9.

Masuala yanayochangia kuwepo kwa hali iliyo Yemen ni magumu yakiwemo bei ya juu ya vyakula na mafuta duniani , mizozo pamoja na misukosuko ya kisiasa. Mwaka ujao WFP inapanga kupanua oparesheni zake kwa lengo la kusambaza chakula kwa watu wote milioni tano wanaokabiliwa na hali mbaya ya uhaba wa chakula nchini Yemen.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031