Waziri wa Mauritius ataka kuwepo mshikamano wa pamoja ili kukabiliana na mikwamo ya kiuchumi

Kusikiliza /

Arvin Boolell

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Mauritius Dr. Arvin Boolell amesema kuwa ili dunia ifaulu kukabiliana na mikwamo ya kiuchumi inapaswa kuweka uratibu ambao utaziwezesha taasisi za Umoja wa Mataifa kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi wa dunia.

Waziri huyo ambaye alikuwa akizungumza kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema kuwa kwa kadri mataifa yatakavyojitahidi kukabiliana na mikwamo ya kiuchumi hayawezi kufaulu vya kutosha kama taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa hautapewa zingatio la kuratibu mwenendo wa uchumi wa dunia.

Mwanadiplomasia huyo hata hivyo alitupia mkono wa pongezi baraza la uchumi na masula ya kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC na alitaka mataifa wanachama kuendelea kuliunga mkono.

Pamoja na eneo hilo, pia hotuba ya kiongozi huyo alimulika maeneo yanayohusu tatizo mtambuka la kukosekana kwa ajira miongoni mwa vijana, machafuko yanayoendelea Syria na mkwamo wa kisiasa nchini Madagascar.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031