Wahamiaji wa Afrika waliokwama nchini Morocco kusafirishwa nyumbani:IOM
Kusikiliza /Zaidi ya wahamiaji 1000 kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara kwa sasa ambao wamekwama nchini Morocco watasafirishwa kwenda nchi zao kupitia kwa mpango unaotarajiwa kuongozwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.
IOM inasema kuwa wahamiaji hao wengi kutoka Cameroon , Nigeria, Senegal na Ivory Coast huunda walisafirishwa kiharamu kwenda Morocco kwa minajili ya kusafirishwa hadi Ulaya lakini sasa hivi wamekwama nchini Morocco bila ya ajira na mahali pa kuishi. Kati ya wahamiaji wamo watoto wasio na wazazi, wanawake wajawazito na wanawake walio na watoto wachanga. IOM inasema kuwa inahitaji karibu dola milioni moja kwenye programu hiyo. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.
(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)
