Watu maskini wanahitaji kupata haki ili kukabiliana na umaskini: UM

Kusikiliza /

Magdalena Sepulveda

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini wa kupindukia, Magdalena Sepúlveda, ametoa wito kwa serikali kote duniani kuchukua hatua mara moja kuhakikisha watu maskini zaidi wanapata haki, katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini.

Bi Sepulveda amesema kuwa na uwezo wa kupata haki kwenyewe ni haki ya binadamu, na kusema kuwa kila serikali inapaswa kuendeleza uwezo huo kwa watu maskini zaidi, kama sehemu ya jitihada za kukabiliana na umaskini.

Hafla ya maadhimisho ya siku hii ya kutokomeza umaskini ni inafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, chini ya kauli mbiu "Kukomesha ukatili wa umaskini wa kupindukia: kuwapa watu uwezo na kujenga amani."

Hafla hiyo imeandaliwa na kwa ushirikiano wa idara ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii, DESA, na shirika la International Movement ATD Fourth World, pamoja na ujumbe wa Ufaransa na Burkina Faso kwenye Umoja wa Mataifa. Christina Diez ni mwakilishi mkuu wa International Movement ATD 4th world kwenye Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA CHRISTINA DIAZ)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031