Watoto wanaoishi ukimbizini wana haki ya kupata elimu: EU

Kusikiliza /

watoto nchini Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limepata zaidi ya Euro Milioni Nne na Nusu kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya mradi wake wa dharura wa elimu kwa watoto wa Syria wanaoishi ukimbizini nchini Jordan pamoja na watoto wa jamii zinazotoa hifadhi.

Msaada huo wa hivi karibuni unafanya mchango wa EU kufikia jumla ya Euro Milioni Kumi mwaka huu kwa mpango huo na umetangazwa wakati wa ziara ya pamoja kati ya Rais wa Tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso na Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Anthony Lake katika shule mpya kwenye kambi ya wakimbizi ya Za'atari kaskazini mwa Jordan.

Barroso amesema wanapaswa kuhakikisha watu waliokimbia makazi yao wanaishi maisha ya staha na watoto wao hawapotezi haki yao ya msingi ya kupata elimu na maisha bora ya baadye.

Kwa upande wake Mkuu wa UNICEF amesema shule hizo zinaweza kuwa chemchem ya amani kwa watoto wa Syria ambao wamekumbwa na maisha ambayo mtoto hapaswi kukumbana nayo.

Fedha hizo zilizotolewa zitasaidia mafunzo ya walimu pamoja na mishahara, ada za shule na vifaa vya shule na gharama zingine kwa miaka 2011/2012 na 2012/2013.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930