Wataalam wa UM washangazwa na mauaji ya mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Honduras

Kusikiliza /

Margaret Sekaggya

Wataalam watatu wa Umoja wa Mataifa wameelezea kushangazwa kwao na mauaji ya mwanasheria wa kutetea haki za binadamu Antonio Trejo Cabrera katika taifa la Honduras, na kukitaja kama kitendo kisichokubalika kamwe, huku kukiwepo hofu kubwa kuhusu usalama wa wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo, hususani wale wanaoshughulikia masuala ya mizozo ya ardhi kwa njia ya amani.

Wataalam hao watatu maalum ni Margaret Sekaggya, anayehusika na hali ya wateteaji wa haki za binadam; Christof Heyns, ambaye anahusika na mauaji kinyume na sheria na Frank LaRue, ambaye anahusika na uhuru wa kujieleza.

Antonio Trejo Cabrera, ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kupinga madai ya ukiukaji wa sheria unaotekelezwa na wamiliki wa ardhi na wanasiasa, aliuawa kwa kupiga risasi mara tano mnamo tarehe 2 Septemba. Wataalam hao wameitaka serikali ya Honduras iweke mfumo wa kitaifa wa kuwalinda wanaotetea haki za binadam haraka iwezekanavyo, na kuwachukulia hatua za kisheria wanaotekeleza uhalifu kama huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930