Wanawake wa vijijini ndio wazalishaji wakubwa zaidi wa chakula duniani:Ban

Kusikiliza /

wanawake vijijini

Wanawake wa vijijini ndio huzalisha asilimia kubwa ya chakula, ndio hutunza mazingira kusaidia katika kupunguza hatari ya majanga miongoni mwa jamii zao. Hii ni kwa mujibu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake wa vijijini inayoadhimishwa tarehe 15 mwezi oktoba kila mwaka.

Ban amesema kuwa changamoto kubwa ambayo kwa sasa inawakabili asimilia kubwa ya wanawake walio vijijini ni kuwa hawana umiliki wa ardhi wanayolima na mara nyingi huwa wananyimwa huduma za kifedha zinazostahili kuwainua kutoka kwenye umaskini ili wapate kuishi bila ya kutatizwa na huduma zikwemo za afya, maji safi na usafi.

Ban amesema kuwa kuwaunga mkono wanawake wa vijijini ni muhimu katika kuangamiza umaskini na njaa lakini kuwanyima wanawake hao haki zao ni sawa kuwanyima watoto wao na jamii maisha mema ya baadaye. Katibu mkuu ameongeza kuwa wakati usalama wa lishe na chakula vinapoimarishwa wanawake wa vijini huwa na fursa za kupata ajira na kuwawezesha kukidhi mahitaji ya watoto wao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031