Ban ahuzunishwa na mauaji ya walinda amani Darfur

Kusikiliza /

kikosi cha UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea huzuni na mshangao wake kufuatia mauaji ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa yalotokea Jumanne jioni katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan. Watu wasojulikana waliwaua wanajeshi wanne, na kuwajeruhi wengine wanane baada ya kuuvizia msafara wa askari wa Nigeria walinda doria, katika eneo la El Geneina.

Bwana Ban ametoa wito kwa serikali ya Sudan kufanya uchunguzi na kuhakikisha walotekeleza shambulizi hilo wanakabiliwa na mkono wa sheria. Awali, Kamanda wa kikosi cha UNAMID ambaye pia sasa anasimamia ujumbe wa UNAMID, Luteni Jenerali Patrick Nyamvumba, alitoa ujumbe kama huo, na kulaani vikali shambulizi hilo dhidi ya walinda amani hao.

Katibu Mkuu ametuma pia ujumbe wa rambirambi kwa serikali ya Nigeria na familia za walofariki katika shambulizi hilo, ambalo lilifanyika yapata kilomita mbili tu kutoka kwenye makao makuu ya UNAMID Darfur.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031