Wakimbizi wa Syria wajiandaa kwa msimu wa baridi

Kusikiliza /

baridi, Syria

Mashirika ya Umoja wa Mataifa wanakusanya misaada ambayo itasaidia zaidi ya wakimbizi 340,000 wa Syria kukabiliana na msimu wa baridi unaokuja. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa wakimbizi walio nchini Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq watahitaji mahema, nguo za joto, mablanketi mazito, mafuta pamoja na chakula na maji.

Melissa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa shirika hilo litahitaji karibu dola milioni 64 kwa maandalizi ya msimu wa baridi na pia kuwahudumia wasyria milioni 1.2 waliolazimika kuhama makwao ndani mwa nchi.

"Ninafikiri hatuko kwenye hali nzuri ya maandalizi. Tumetabiri idadi ambayo ni muhimu , 700,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka. Ikiwa tutafuata mpango huu tunaweza kuhisi vizuri kwa watu wanaopata joto na faraja msimu wa baridi. Kile tunachofanya kwa wakimbizi wa ndani hakijatosha. Huduma za kibinadamu ni suala kubwa. Uwezo wetu wa kuwafikia wenye mahitaji unatatizwa na ghasia. Watu tunaowafikia wako mijini tuliko na ofisi. Lakini watu walio nje ya sehemu za opareshini ni vigumu. Chama cha mwezi mwekundu cha Syria kinafanya jitihada za kuwafikia watu kwenye sehemu ambazo Umoja wa Mataifa hautafika."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031