Wakimbizi wa Kipalestina wauawa nchini Syria

Kusikiliza /

wakimbizi wa kipalestina walioko Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limerejelea kauli yake ya kuitaka Syria kuweka ulinzi wa kutosha kwa wakimbizi wa kipalestina pamoja na raia wengine dhidi ya mapigano yanayoendelea nchini humo.

Wito huo unafuatia shambulio la Ijumaa asubuhi kwenye kambi ya wakimbizi ya Neirab Kaskazini mwa Syria lililosababisha vifo vya wapalestina wanne na majeruhi watano.

UNRWA imelaani vifo hivyo ikisema vingeweza kuepukika na imetaka kila pande katika mgogoro nchini SYRIA kujiepusha kushambulia maeneo ya raia na kwamba pande hizo zizingatie wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

Kambi ya Neirab iliyo jirani na Uwanja wa ndege wa Aleppo nchini Syria ni makazi ya takribani wakimbizi Elfu Ishirini na Wawili wa kipalestina na tangu mwezi Juni eneo hilo limekuwa likiathiriwa na mapambano kati ya vikosi vya serikali na waasi nchini humo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031