Wakimbizi wa Iraq waenda Ujerumani kuanza maisha mapya: IOM

Kusikiliza /

wakimbizi wa Iraq

Kundi la wakimbizi wa Iraq wapatao 105 wakiwa na familia zao wamesafirishwa kwa ndege hii leo kuelekea nchini Ujerumani ambako wanatazamia kuanzisha maisha mapya katika eneo la Hanover.

Wakimbizi hao ambao walikuwa wakiishi katika kambi mbalimbali ikiwemo zile za Kayseri, Bilecik walifuzu mahojiano yaliyoendeshwa na maafisa uhamiaji wa Ujerumani mapema mwezi July mwaka huu.

Mjini Hanover wanatazamiwa kupokelewa na ujumbe utakaongozwa na waziri wa mambo ya ndani Dr. Hans-Peter Friedrich.Mapema kabla ya kuanza kwa safari yao, walifanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Nchini Ujerumani katika siku zao za mwanzo watakuwa kwenye vituo maalumu kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa kijerumani na baadaye watatawanywa katika maeneo yaliyoanishwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031