Wachunguzi wa UM watafuta kibali kuingia Syria

Kusikiliza /

Paulo Pinheiro

Jopo la Tume ya Umoja wa Mataifa linalochunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria, limemwandikia barua Rais Bashar Al-Assad wa Syria ya kuomba kuwa na mazungumzo naye, ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu tume hiyo kuundwa lakini haijaweza kupata kibali kuingia nchini humo kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mwenyekiti wa tume hiyo Paulo Pinheiro amesema ana matumaini kuwa watakutana na Rais Assad kujadili ombi la tume yake kuingia nchini humo.

Katika ripoti yake kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa mataifa mwezi Septemba mwaka huu, tume hiyo ilieleza kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu unaoweza kusababisha vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu unafanywa na majeshi ya serikali na vikundi vya upinzani.

Bwana Pinheiro amesema tayari tume yake imeandaa orodha ya watu ambao wanatuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita nchini Syria.

"Hatuwezi kutabiri hali ya baadaye. Sifahamu iwapo atatukubali. Lakini ni wajibu wetu kuingia nchini humo. Tunafikiri ni muhimu kuzungumza na mtu anayehusika. Tunatarajia kwenda kumuona Rais Assad bila masharti yoyote na kujadili jinsi Tume yetu itakavyoingia Syria. Sisi ndio tunaohusika na ufuatiliaji wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Sisi sio mahakama, wala siyo chombo cha kushtaki makosa ya jinai. Kile tunachofanya ni kupata ushahidi kwa ajili ya hatua za baadaye za kimahakama ili wanaokiuka haki wawajibishwe."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031