Waathiriwa wa mafuriko nchini Pakistan waanza kupokea misaada

Kusikiliza /

mafuriko nchini Pakistan

Karibu watu milioni 5 wameathiriwa na mafuriko kwenye mikoa ya sindh, Punjab na Balochistan nchini Pakistan kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA. Mafuriko hayo yaliayoanza karibu mwezi mmoja uliopita yamesababisha zaidi ya ekari milioni moja ya ardhi ya kilimo kuzama na kuua karibu mifugo 10,000.

OCHA inasema kuwa kutokana na kiasi kikubwa cha maji yaliyoterema kwenye mikoa iliyoathirika , huenda maji hayo yakachanganya na vyanzo vya maji na kusababisha mikurupuko ya magonjwa. Zaidi ya watu 260,000 wamehama makwao na sasa wanaishi kwenye kambi. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA mjini Geneva.

"Kinachohitajika kwa sasa ni chakula, makao ya dharura, maji safi na huduma za usafi. Kwenye awamu ya kwanza ya kutoa huduma watu 140,000 walioathiriwa wamepokea chakula kwenye mikoa ya sindh na Balochistan huku mashirika ya kibinadamu yakisambaza madawa kwa karibu watu 450,000 kwenye maeneo yaliyofuriko. Balochistan, Punjab na Sindh ndiyo mikoa iliyoathirika zaidi wakati huu. Nyingi ya wilaya zilizoathirika hasa Balochistan na Sindh waathiriwa walikuwa wakijaribu kurejea hali ya kawaida kutoka kwa mafuriko ya mwaka 2010 na 2011."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031