Watetezi wa haki za binadamu Iran watiwa matatani:UM

Kusikiliza /

Rupert Colville

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za binadamu imeonyesha wasiwai juu ya hali ya kuendelea kutiwa matatani kwa watetezi mashuhuri wa haki za bindamu, waandishi wa habari na hata wanaharakati wa kisaisa nchini Iran na kueleza kuwa kitendo hicho ni ukandamizaji wa sauti za umma..

Afisa kutoka ofisi hiyo Rupert Colville amesema vitendo vya kuendelea kuwakamata na kuwatishia wanaharakati na waandishi wa habari vinatia wasiwasi hususan wakati kipindi hiki cha kuelekea uchagzi wa Rais mwakani ambapo amewataja waliokumbwa na mkasa huo kuwa ni pamoja na Mohammad Ali Dadkha kutoka kituo cha utetezi wa haki za binadamu aliyekamatwa tayari kuanza kifungo cha miaka Tisa jela alichohukuwa awali baada ya kupatikana na hatia ya kuwa mwanachama wa kikundi kilichotaka kupindua serikali ya Iran.

Mwingine ni Mkuu wa shirika la habari la Uingereza,  Iran Parisa Hafezi anayeshikiliwa kwa madai ya kusambaza taarifa za uongo na propaganda.

"Wanasheria, watetezi wa haki za binadamu na vyombo huru vya habari wana mchango mkubwa katika jamii za kidemokrasia na hivyo wanapaswa kuwa huru kufanya kazi zao bila vitisho, manyanyaso yoyote au kushtakiwa. Vitendo vya wao kukamatwa, na kuhukumiwa ni taswira dhahiri yenye lengo la kudhibiti uhuru wa kujieleza, kutoa mawazo ambao unaelezwa bayana katika mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisaisa ambao Iranni mwanachama. Tunaiomba Iran kuwaachia mara moja wale wote waliokamatwa wakitekeleza haki zao za kimsingi kwa amani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031