Viwango vya juu vya madeni kwa nchi maskini vyamtia hofu Jeremić

Kusikiliza /

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremić.

Nchi zilizoendelea zinapaswa kutekeleza ahadi zao za kusaidia kiuchumi nchi zinazoendelea na hiyo ni kauli ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Vuk Jeremic aliyoitoa mbele ya kikao cha barazahilojijiniNew York, Marekani.

Bwana Jeremic akizungumza kwenye mkutano wa shirika la kimataifa la biashara na mandeleo, UNCTAD, ameonya kwa kutofanya hivyo viwango vya madeni kwa nchi hizo maskini vitakuwa vikubwa kupindukia na kuhatarishwa kushindwa kukopesheka.

Ameelezea wasiwasi wake juu ya uwezo wa nchi maskini kushughulikia madeni wakati ambapo bado kuna madhara ya mdororo wa kiuchumi duniani.

Amesema baadhi ya majumuisho ya tafiti za hivi karibuni za UNCTAD kuhusu usaidizi kwa nchi zinazoendelea yanatia wasiwasi ambapo ametoa mfano kuwa majumuisho hayo yanaeleza kuwa mikakati katika muongo uliopita ya kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi ilihusisha matumizi makubwa ya akiba ya fedha na hivyo akiba hizo bado hazirejeshwa na kufikia viwango vya awali.

Hivyo basi Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema suluhisho ni ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea huku akizitaka nchi zilizoendelea nazo kuendeleza mshikamano wao na nchi maskini zinazokabiliwa na madeni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031