Valarie Amos azuru Benin, na kuelezea changamoto ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Kusikiliza /

Valerie Amos

Mkuu wa huduma za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amehimiza kuwepo mabadiliko katika wakati ambapo jumuiya ya kimataifa ikijishughulisha na utoaji wa huduma za dharura ikiwemo pia kuipiga jeki serikali ya Benin inayokabiliwa na hali ya kuwakwamua raia wake waliokumbwa na mafuriko.

Bi Valarie Amos amesema kuwa lazima kuchukuliwe njia mujarabu kuwataarifa wananchi wa eneo hilo namna wanavyopaswa kuwa tayari kukabiliana na matukio yasabishwayo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo pia matukio ya mafuriko.

Akizungumza mjini Cotonou mji mkubwa zaidi nchini Benin Bi Amos amesema kuwa ni vigumu kusema kuwa jamii ya kimataifa inaweza kuzuia matukio kama mafuriko lakini jambo la kutia matumaini ni kwamba jamii hiyo inauwezo wa kutoa elimu kuhusiana na madhara ya hali hiyo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Mkuu huyo wa OCHA yuko nchini humo kwa mwaliko wa rais wa Benin Boni Yayi kufuatia maafuriko makubwa yaliyoikumba taifa hilo.Akiwa nchini humo anatazamiwa kukutana na jamii ya watu waliolazimika kuhamia sehemu nyingine kutokana na maeneo yao kuathiriwa na mafuriko.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031