Uteuzi wa Waziri mkuu wa Somalia waungwa mkono na UM

Kusikiliza /

Augustine Mahiga

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amempongeza waziri mkuu wa nchi hiyo Abdi Farah Shirdon na kumshauri aweze kubuni serikali iliyo ya kuwajibika na yenye uwazi. Balozi Agustine Mahiga amesema kuwa uteuzi wa Waziri mkuu mpya ni hatua nyingine nchini humo kwenye mpango wa amani.

Uteuzi huo wa Waziri mkuu mkuu utapelekwa bungeni kuidhinishwa ili aweze kupata fursa ya kuunda baraza la mawaziri ambalo pia litaidhinishwa na bunge. Mahiga ameahidi uungwaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa bwana Shirdon na kumpa moyo wa kuanza maramoja jihada za kujenga serikali yenye uwazi, iliyojitolea na yenye kuwajibika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930