Urusi yatoa mfano wa chombo cha Satelaiti kwa makao makuu ya UM mjini Vienna

Kusikiliza /

satelite, UM

Urusi imetoa mfano wa chombo cha satelaiti kwa Umoja wa Mataifa, ambacho kitawekwa hadharani kwenye sehemu ya maonyesho ya vyombo vya safari za anga za juu katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Vienna, Austria. Chombo hicho kimewasilishwa na Naibu Mkuu wa shirika la safari za angani la Urusi, Roscosmos, na kushuhudiwa na mkuu wa afisi ya Umoja wa Mataifa mjini Vienna, Yury Fedotov.

Fedotov ameshukuru kwa msaada huo uliotolewa leo ikiwa ni siku ya kwanza ya maadhimisho ya wiki ya kimataifa ya masuala ya anga za juu ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la linalohusika na mambo ya anga za juu UNOOSA husherehekea kuanzia tarehe Nne hadi Kumi Oktoba ya kila mwaka.

Amesema matumizi bora ya teknolojia ya satelaiti husaidia watumiaji wengi duniani katika shughuli za kiraia, kisayansi na hata kibiashara.

Mkurugenzi wa UNOOSA Mazlan Othman amesema wiki ya kimataifa ya anga za juu hutoa fursa ya kutathmini nafasi ya sayansi na teknolojia katika kuimarisha maisha ya binadamu na kulifanya anga la juu ambalo ni la kufikirika zaidi kuwa karibu na la manufaa zaidi kwa binadamu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031