UNHCR yataka nchi ziache mipaka wazi kwa ajili ya wakimbizi

Kusikiliza /

Antonio Guterres

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Antonio Guterres amerejelea wito wake wa kutaka nchi ziache mipaka yao wazi kwa ajili ya kupokea watu wanaokimbia migogoro na majanga mbali mbali duniani kote.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva , Uswisi, Guterres amesema UNHCR hivi sasa imezidiwa uwezo wa kuwapatia hifadhi na msaada wakimbizi na watu waliopoteza makazi ndani ya nchi zao, na kwamba shirika hilo linahitaji fedha zaidi.

Ametoa mfano wa migogoro ya sasa inayotokea kwa wakati mmoja huko Syria , Sudan , Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Mali ambayo amesema yote inalazimu UNHCR kwa na fedha kusaidia wakimbizi huku bado kuna wakimbizi wengine wanaohitaji msaada..

Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa UNHCR amesema shirika lake linalazimika kupunguza usaidizi katika miradi mingine ili kushughulikia mambo ya dharura.

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031