UNHCR yapongeza Ecuador, Honduras na Ureno kwa kusaini mkataba wa kuwasaidia watu wasio na uraia

Kusikiliza /

Jose Filipe Moraes Cabral, Mary Elizabeth Flores na Gabriele Goettsche-Wanli

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameyapongeza mataifa ya Ecuador, Honduras na Ureno kwa kujiunga kwenye mtandao wa mataifa ambayo yamechukua hatua za kukabiliana na suala la ukosefu wa uraia.

Mataifa yote hayo matatu yaliusaini mkataba wa kuwatambua watu wasio na uraia wa taifa lolote katika hafla maalum iliyoandaliwa wakati wa mkutano wa Baraza Kuu mjini New York. Ecuador iliusaini mkataba wa 1961 wa kupunguza ukosefu wa uraia, Honduras ikatia saini ule wa 1954 unaohusiana na hali ya watu wasio na uraia, na Ureno ikaitia saini yote miwili.

Kamishna Guterres amesema hatua iliyochukuliwa na mataifa hayo matatu inaonyesha kuendelea kuwepo utambuzi wa suala la ukosefu wa uraia, na hiari ya kisiasa ya kulishughulikia, akitaja kuwa hali hiyo inawaathiri hadi watu milioni 12 kote duniani. Amesema wengi wao hawana usalama katika nchi wanamoishi, hunyimwa haki ya kuwa na ajira, na hawapati huduma zote za afya na elimu. George Njogopa na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031