UNESCO na EU kushirikiana katika Elimu, Utamaduni, Sayansi na haki za binadamu

Kusikiliza /

Irina Bokova na Andris Piebalgs

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na Umoja wa Ulaya EU, zimeingia makubaliano mapya ya kubadilishana taarifa na kuimarisha ushirikiano wako katika nyanja za elimu, utamaduni, Sayansi na haki za binadamu.

Makubaliano yametiwa saini kati ya Mkuu wa UNESCO Irina Bokova, Makamu Rais wa EU Catherine Ashton na kamishna wa maendeleo wa EU Andris Piebalgs.

Akizungumza baada ya utiaji saini, Bokova amesema hatua hiyo siyo tu ni fursa ya kurejelea ushiriki wa EU katika mipango ya UNESCO bali pia kwa misingi ambayo UNESCO inazingatia na kutambuliwa pia na Umoja huo huku Pielbags akisema kuwa ushirikiano huo unafanya kazi kuwa bora zaidi .

Makubaliano hayo yanaweka bayana vipaumbele vya kimkakati na unahamasisha kuongezeka kwa mashauriano ya kisera kati ya taasisi hizo kwenye masuala yenye maslahi ya pamoja kama vile elimu, utamaduni, sayansi na teknolojia, sera usafiri wa majini na uhuru wa kujieleza .

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031