UNAIDS yahimiza wajibu wa pamoja kufadhili mahitaji ya UKIMWI katika nchi zinazoongea kifaransa

Kusikiliza /

UKIMWI

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na UKIMWI, UNAIDS, limehimiza wajibu wa pamoja katika kukabiliana na upungufu wa ufadhili kwa mahitaji ya UKIMWI katika nchi zinazoongea lugha ya kifaransa. Ripoti mpya ya UNAIDS inaonyesha kwamba hatua zimepigwa katika nchi zinazoongea kifaransa, lakini bado kuna upungufu katika kuitikia tatizo la UKIMWI, na hivyo kutoa wito kwa mataifa na wafadhili kuongeza uwekezaji katika kukabiliana na UKIMWI.

Ripoti hiyo inayohimiza kufanywe uamuzi sasa wa kukomesha maambukizi mapya ya HIV, na ubaguzi katika matibabu, inaonyesha tofauti katika hatua zilizopigwa kwenye nchi hizo, na mwendo wa pole uliopo kusini mwa jangwa la Sahara, hasa katika kuzuia maambukizi mapya miongoni mwa watoto na kuongeza kasi ya huduma za matibabu.

Jumla ya dola bilioni 2.6 billion zitahitajika kila mwaka, hadi mwaka 2015, kufadhili mahitaji ya UKIMWI katika nchi za francophonie zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, kwa mujibu wa ripoti hiyo, ambayo imetolewa kabla ya mkutano wa 14 wa La Francophonie mjini Kinshasa, DRC.

Akizungumza wakati wa kutolewa ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa ushirikiano wa nchi za francophonie, Abdou Diouf, amesema kuwa kikomo cha ugonjwa wa UKIMWI duniani kinaweza kufikiwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031