Umoja wa Mataifa kushiriki kampeni ya kutoa chanjo Afrika

Kusikiliza /

ugonjwa wa uti wa mgongo

Zaidi ya watu Milioni 50 katika nchi saba za Afrika watapatiwa chanjo ya homa ya uti wa mgongo katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, ikiwa ni kampeni ya pamoja inayohusisha ushirikiano wa kimataifa wa utoaji chanjo, Gavi, shirika la afya duniani, WHO, shirika la kuhudumia watoto wa la Umoja wa Mataifa, Unicef na mradi wa chanjo dhidi ya homa ya uti wa mgongo.

Mkuu wa Gavi, Dkt. Seth Berkely amesema hatua hiyo inatokana na kwamba ugonjwa huo unaoweza kusababisha kifo ndani ya saa Arobaini na Nane uko hatarini kulipuka katika nchi hizo ambazo ni Benin , Cameroun , Chad , Ghana , Nigeria , Senegal na Sudan .

Amesema kampeni hiyo itahakikisha walio hatarini kukumbwa na homa ya uti wa mgongo wakiwemo watoto na vijana wanakuwa wamepatiwa kinga ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

"Hakuna anayefahamu kwa nini mlipuko wa ugonjwa huu homa ya uti wa mgongo ni katika ukanda huo tu. Kila baada ya miaka mitano hadi Saba ugonjwa huo unalipuka na idadi ya wagonjwa inakuwa kama siyo maelfu basi mamilioni. Na hali hiyo inakwamisha kabisa uchumi. Vituo vya tiba vinaanzishwa kwa ajili ya kutoa tiba kwa watu wengi na kama mtu hatakufa, anabakia hali lakini bado anakuwa ameathirika sana. Unakuta kuna mtoto kiziwi, mwenye uvimbe katika ubongo na matazito mengine mengi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031