UM yasema kuna uwezekano watoto waliuwawa wakati wa shambulizi la anga la vikosi vya kimataifa Afghanistan

Kusikiliza /

Leila Zerrougui

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unatiwa shaka juu ya mwenendo wa vikosi vya kimataifa nchini Afghanistan kufuatia kuwepo uwezekano wa watoto watatu kuwa ni miongoni mwa waliopoteza maisha baada ya vikosi hivyo vya kimataifa kufanya shambulizi la angani .

Katika taarifa yake msaidizi wa Katibu Mkuu juu ya masuala ya watoto na maeneo yenye mizozo Leila Zerrougui amesema kuwa matukio kama hayo yanaendelea kuwacha watoto wengi katika mazingira magumu na kuwa kwenye mtego wa kunasa wakati wote.

Kulingana na kikosi cha usalama cha Umoja wa Mataifa ISAF shambulizi la angani lililofanywa siku ya jumapili huko kusin mwa Afghanistan ambalo liliwalenga wafuasi wa Taliban liliwauwa watoto watatu.

Ripoti zinasema watoto hao walikutwa na maafa hayo wakati wakiwa wakikusanya kuni katika eneo la jirani kulikofanyika shambulizi hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031