UM wataka sekta ya posta kubanua uwigo wake

Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa umelitaka shirika la posta duniani kupanua huduma zake ili kuwafikia wateja wengi zaidi wanakuwa na ukosefu wa huduma za kifedha.

Wito huo umetolewa katika chapisho jipya lililotolewa na Umoja wa shirika la posta duniani UPU. Ripoti hiyo imesema wakati dunia ikiendelea kushuhudia mabadiliko makubwa, lakini bado kuna idadi kubwa ya wananchi ambao hawana huduma za uhakiki za kibenki.

Ripoti hiyo imebainsha kuwa maelfu ya watu duniani wameachwa kando na mifumo inayounganishwa na taasisi za kifedha hivyo kwa benki hiyo kuboresha huduma zake kutawafaidia wengi.

Ripoti hiyo inatolewa katika wakati zaidi ya wajumbe 2,000 wakikutana huko Doha, Qatar kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wa posta ambao pamoja na mambo mengine unaangazia changamoto inazoziandama sekta ya posta.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031