UM wasifu jitihada za Tanzania kupunguza vifo vya akina mama wajawazito

Kusikiliza /

Michael Bloomberg; Ban Ki-moon; Jakaya Kikwete; Helen Agerup

Tanzania imeripotiwa kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na kufikia idadi ya chini zaidi katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, na hiyo ni kutokana na utekelezaji wa miradi ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema hayo leo jijini New York Marekani wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mpango wa ubunifu wa afya ya wajawazito nchini Tanzania uliotekelezwa kwa miaka mitatu chini ya ufadhili wa Meya wa New York Michael Bloomberg.

Mpango huo unaoratibiwa na Umoja wa Mataifa umepata shime zaidi hii leo baada ya Bloomberg kuridhishwa na utekelezaji wake na kutangaza dola Milioni Nane kwa miaka mitatu ijayo huku taasisi ya H & B ya Helen Agerup ikiunga mkono kwa kutoa dola Milioni Saba na Nusu kwa mradi huo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametoa shukrani na kuelezea vile ambavyo serikali yake ilianza kuchukua hatua za kisera kwa afya ya wajawazito na hatimaye kupata msaada zaidi.

(SAUTI YA RAIS KIKWETE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031