UM wapongeza makubaliano ya amani Philippines

Kusikiliza /

Leila Zerrougui

Umoja wa Mataifa umesema kuwa umekaribisha kwa matumaini makubwa hatua iliyochukuliwa na serikali ya Philippens iliyotiliana saini makubaliano ya amani na kikosi cha waasi cha Moro Islamic Liberation Front (MILF) na hivyo kuzika hali ya vita na uhasama uliodumu kwa miongo kadhaa.

Makubaliano hayo yanafungua njia kupatikana kwa amani ya kudumu katika eneo la Kusin mwa kisiwa cha Mindano kilichopigania kujitenga kwa muda mrefu.

Katika taarifa yake juu ya hatua hiyo,Mwakilishi wa Katibu Mkuu juu ya masuala ya watoto na maeneo yanayokumbwa na mizozo, Leila Zerrougui, alipongeza hatua hiyo ambayo amesema kuwa siyo tu yanaleta mustakabala mwema kwa wananchi wa eneo hilo lakini pia makubaliano hayo yanafungua njia kwa maisha ya mamia ya watoto ambao waliathiriwa pakubwa na mapigano hayo.

Mapema mwezi huu rais wa Philippines Benigno Aquino alitangaza kuwa serikali yake imefikia makubaliano ya awali na kundi la MILF ambalo lilianzisha mapigano miongo kadhaa iliyopita kwa likitaka kujitenga na dola ya Philipines.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930