UM wapongeza hali ya amani nchini Sierra Leone

Kusikiliza /

kugiga kura

Ikiwa ni takribani mwezi Mmoja na Nusu umebakia kabla Sierra Leone haijafanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, Umoja wa Mataifa kupitia Tume ya kujenga amani imepongeza maendeleo thabiti ya maelewano nchini humo na kusisitiza umuhimu wa uongozi wa kitaifa na msaada wa kimataifa ili kuepusha vitisho vyovyote vinavyoweza kurejesha mzozo nchini humo. Taarifa zaidi kutoka kwa

(RIPOTI YA…)

 

Kikao cha Tume hiyo ya kujenga amani ya umoja wa Mataifa kimefanyika mjini New York , Marekani Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo wajumbe walipongeza maendeleo ya amani na utulivu yaliyofikiwa sasa kabla ya uchaguzi mkuu tarehe 17 mwezi ujao.

 

Pongezi hizo zimetolewa baada ya tathmini ya pili ya matokeoya kikao cha ngazi ya juu cha tume hiyo kuhusu Sierra Leona na kupendekeza kuwa serikali isimamie masuala ya amani na utawala bora.

 

Katika kujenga umoja, serikali ya Sierra Leone imetakiwa kushirikisha pande zote nchini humo, kuweka mfumo huru wa kuwasilisha malalamiko dhidi ya polisi, kuendeleza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa bila kusahau kusaidia tume ya taifa ya uchaguzi na ile ya kusajili vyama vya siasa.

 

Vyama vya siasa na vyombo vya habari kwa pamoja wametakiwa kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia makubaliano ya awali ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani huku washirika wa kimataifa wakitaka kusaidia mkakati wa kitaifa wa mabadiliko nchini Sierra Leone .

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone Joseph Dauda ameihakikishia Tume hiyo kuwa serikali yake itahakikisha uchaguzi huo mkuu ambao kampeni zinaanza tarehe 15 mwezi huuu unakuwa huru na wa haki.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031