UM na Umoja wa Afrika zakubaliana kushiriki kikamilifu mchakato wa amani Darfur

Kusikiliza /

Kaimu Mkuu wa UNAMID Aïchatou Mindaoudou na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkhosazana Dlamini-Zuma.

Kaimu Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hukoDarfur, UNAMID, Aïchatou Mindaoudou amesisitiza umuhimu wa Umoja wa Afrika kushiriki kikamilifu katika kuendeleza harakati za kuleta amani na utulivu kwenye eneo hilo la Darfur huko Sudan.

Mindaoudou amesema hayo wakati wa mazungumzo yake mjini Addis Ababa, Ethiopia na Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkhosazana Dlamini-Zuma ambapo pamoja na mambo yanayohusu mchakato wa amani wa Darfur, walijadili kurejea upya kwa ghasia kaskazini mwa jimbo hilo mwezi Agosti.

Viongozi hao pia walijikita zaidi katika makubaliano ya hivi karibuni ya  Doha,Qatarkati ya serikali yaSudanna kikundi kimoja cha waasi huko Darfur, JEM pamoja na maandalizi yanayoendelea ya mkutano wa wahisani kwa ajili ya Darfur ambao pia utafanyikaDoha, mwezi Disemba.

Pia Kaimu Mkuu huyo wa UNAMID aligusia mauaji ya hivi karibuni ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa ambapo Bi. Dlamini-Zuma amesema atawasilisha yote waliyojadili mbele ya Tume ya Umoja wa Mataifa na kuahidi kufuatilia kwa karibu suala la Darfur.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031