Homa ya Marburg yaua watu watano nchini Uganda: WHO

Kusikiliza /

homa ya Marburg, Uganda

Homa ya Marburg yaua watu watano nchini Uganda: WHO

Mwakilishi wa shirika la Afya duniani WHO nchini UGANDA, Dkt. Joaquim Saweka, amesema watu watano wamekufa kutokana na ugonjwa wa homa ya Marburg uliolipuka katika wilaya ya Kabale, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Dkt. Saweka akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa amesema waliokufa ni kati ya wagonjwa Tisa ambapo kwa sasa wagonjwa wane wanapatiwa matibabu na uchunguzi zaidi unaendelea.

"Hii ni bahati mbaya kwa sababu mlipuko huu umetokea siku Kumi na tano tu hivi baada ya kutangaza kumalizika mwa mlipuko wa Ebola. Lakini ni tofauti. Ni kusini-magharibi mwa Uganda na mpaka sasa wagonjwa watano kati ya Tisa wamefariki dunia. Kwa sasa tnafuatilia wagonjwa wengine 34. Hivyo ndivyo hali ilivyo kwa sasa. Tunafuatilia uwezekano wa maambukizo mengine, ikiwemo mji mkuu Kampala."

Tayari WHO inashirikiana na Wizara ya Afya nchini Uganda kudhibiti ugonjwa huo ambapo wamepeleka wataalamu kusaidia uchunguzi wa mlipuko na hatua za kudhibiti ikiwemo kufahamu ugonjwa huo ulipoanzia, kuelimisha na kushirikisha umma ambapo tayari vikosi kazi katika ngazi ya wilaya vimeanza kazi zao.

Hata hivyo WHO imesema haijapendekeza kizuizi cha usafiri au biashara nchini Uganda kutokana na mlipuko huo wa homa ya Marburg.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031