Ufahamu na uwepo wa huduma ni muhimu katika kukabiliana na saratani ya akina mama

Kusikiliza /

saratani ya akina mama

Katika mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, suala moja ambalo liliorodheshwa katika masuala muhimu kujadiliwa lilikuwa saratani, au kansa ya wanawake. Mamilioni ya wanawake kote duniani huathiriwa na saratani ya aina moja au nyingine, mara nyingi zikiwa ni ile ya maziwa ya mama na ile ya mfuko wa uzazi. Akizungumza wakati wa mkutano huo, rais wa Marekani Barrack Obama, alisema juhudi zinapaswa kuangazia kugundua mapema na kuzuia katika vita dhidi ya saratani ya akina mama.

Katika nchi nyingi zinazoendelea, na hasa barani Afrika, ukosefu wa huduma za kupima pamoja na akina mama vijijini kutokuwa na ufahamu kuhusu aina tofauti za kansa huchangia sana matatizo ya ugonjwa huu. Katika makala yetu wiki hii, mwandishi wetu George Njogopa analimlikia suala la saratani miongoni mwa akina mama.

(PKG YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930