Udhibiti wa kisiasa unakiuka uhuru wa kuabudu: Mtaalamu huru UM

Kusikiliza /

Heiner Bielefeldt

Haki ya kuabudu dini na imani yoyote hivi sasa inakiukwa na baadhi ya serikali duniani kwa lengo la kuweka udhibiti wa kisiasa.

Hiyo ni kauli ya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhuru wa kuabudu au imani Heiner Bielefeldt aliyoitoa jijini New York Marekani alipozungumza na waandishi wa habari.

Bwana Bielefeldt amesema moja ya lengo la ukiukwaji wa haki ya uhuru wa kuabudu ni kile alichoeleza kuwa udhibiti wa dini au madai ya ukweli na kushikilia hoja ya umoja wa kitaifa.

“Siasa za kujitambua zina dhima kubwa. Wakati mwingine zinatawala siasa. Kwa hiyo unapokuwa unatawala nchi, waumini wanaweza kuonekana kamawapinzani wanaotekeleza mambo kwa maslahi ya nchi za kigeni. Mawazo kama haya na wakati mwingine ukiukwaji huo wa haki unatokea kwa maslahi ya kisiasa."

Mtaalamu huyo huru wa Umoja wa Mataifa amesema watu wana haki ya kubadilisha imani zao na siyo kulazimishwa kushikilia au kurejea imani zao asili na pia wana haki ya kuwabadili wengine imani zao za dini kwa ushawishi na siyo kwa nguvu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031