Televisheni maarufu ya Israel yakiri kukosea katika tuhuma zake dhidi ya UM

Kusikiliza /

Chris Gunness

Televisheni maarufu zaidi nchini Israel, Channel Two News, imetoa taarifa ya kurekebisha madai ya uwongo iliotoa ikisema makombora yalirushwa kutoka kwenye shule zinazoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, wakati wa vita vya Gaza kati ya mwaka 2008 na 2009.

Taarifa hiyo inaweka wazi kuwa maafisa wa Israel wenyewe walikiri kuwa madai hayo yalikuwa ya uwongo, na kwamba hakukuwa na ushahidi wowote wa kuyaunga mkono.

Msemaji wa UNRWA, Chris Gunness amesema madai hayo ya kupotosha yalikuwepo wakati makombora yaliporushwa karibu na maghala na shule za UNRWA wakati wa vita, lakini maafisa wa Israel wenyewe waliudhihirishia Umoja wa Mataifa kwamba walijua madai ya kuwepo wanamgambo kwenye maeneo ya operesheni za UNRWA yalikuwa ya uwongo. Amesema kurudiwa kwa madai haya ya uwongo mara kwa mara kumeathiri sifa ya UNRWA, na kuchangia uandishi wa habari wenye kupendelea upande mmoja.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031