Tanzania yachukua hatua dhabiti kuboresha afya ya akina mama:Rais Kikwete

Kusikiliza /

rais wa Tanzania na Katibu Mkuu wa UM

Ikiwa imesalia miaka Mitatu kufikia ukomo wa malengo ya Milenia yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani mwaka 2000, Tanzania imeelezwa kuwa imechukua hatua thabiti kutekeleza malengo ya kuboresha afya ya wajawazito pamoja na kupuunguza vifo vya watoto wachanga.

Taarifa hizo za kutia moyo zilitangazwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani wakati wa mkutano wa pamoja baina ya Katibu Mkuu wa Umoja hou Ban Ki Moon, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, Meya wa New York Michael Bloomberg na Mwenyekiti wa Taasisi ya H & B Helen Agerup walipozinda ripoti ya matokeo ya utekelezaji wa mpango wa bunifu wa kupunguza vifo vya wajawazito nchini Tanzania. Mbinu hizo ni pamoja na kutoa mafunzo ya msingi ya uzazi salama kwa watumishi na kujenga vyumba vya kujifungulia maeneo ya vijiji badala ya kwenda mbali.

Mara baada ya uzinduzi huo Radio ya Umoja wa Mataifa ilifanya mahojiano na Rais Kikwete juu ya mafanikio na changamoto katika uzazi salama bila kusahau elimu ambapo kwa kuanza Assumpta Massoi alitaka kufahamu mazingira ya wajawazito kujifungua yako vipi?

(MAHOJIANO NA RAIS KIKWETE))

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031