Taaluma ya ualimu imetekwa:ILO

Kusikiliza /

mwalimu na wanafunzi

Hali mbaya ya uchumi imedhoofisha kwa kiasi kikubwa mazingira ya walimu kufanya kazi na hata mishahara yao . Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani, ILO, Guy Ryder katika taarifa yake aliyoitoa kuelekea siku ya walimu duniani tarehe Tano mwezi huu.

Ryder amesema uhaba wa walimu umesababisha msongamano wa wanafunzi katika darasa wakati huu ambapo bajeti ya sekta ya elimu kwa ajili ya kuboresha huduma na vifaa inapungua siku hadi siku.

Mkuu huyo wa ILO ameenda mbali zaidi na kushutumu vikali kitendo cha kuajiri watu wasio na sifa kuziba pengo la uhaba wa walimu na kusema kuwa wakati umefika kuanza kuzingatia viwango vya juu na kuhakikisha walimu wanaandaliwa vya kutosha katika fani hiyo inayohitaji ujuzi mkubwa.

"Mambo yote haya yamesababisha kuporomoka kwa hadhi ya ualimu. Hii ina maana kwamba watu hawavutiwi na fani hii na hata baadhi ya walimu wanaacha kazi. Tunapaswa kuchukua hatua za harak, mathalani kuanzisha mjadala wenye manufaa wa kijamii kwa lengo la kuinua hadhi ya walimu na kuandaa sera na mikakati itakayovutia watu kuingia katika fani ya ualimu."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031