Suala la ukatili wa ngono wakati wa mizozo

Kusikiliza /

ukatili wa ngono wakati wa mizozo

Wakati kunapotokea mizozo au vita kuna athari ambazo hujitokeza zikiwemo za kuhama kwa watu, uporaji wa mali , mauaji , utekaji nyara na kadhalika. Lakini kuna athari moja ambayo kwa sasa inatajwa kuwa moja ya zana za kivita, na athari hiyo ni ubakaji au dhuluma za kimapenzi hasa kwa wanawake na watoto wasichana.

Katika mjadala wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwezi Septemba, suala hilo la ukatili wa ngono katika mazingira ya mizozo lilijitokeza kama mojawapo ya masuala muhimu ya kujadiliwa na viongozi wa kimataifa.

Makundi kadhaa ya waasi yaliyovitani na serikali zao hususani barani Afrika yanaendelea kutumia tabia hii ya ubakaji au mara nyingine utekaji nyara wa wasichana ambao hutumiwa kama watumwa wa ngono. Ni jambo la kudhalilisha kwa kiasi kikubwa kwa jamii au kwa watu ambao hujipata kutendewa unyama kama huu.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewahi kujipatia sifa ya kuwa makao makuu ya ubakaji kote duniani, kwani mara kwa mara makundi ya waasi huwabaka wanawake kwa viwango vya juu.

Nchini Kenya, wakati wa machafuko yalofuatia uchaguzi wa mwaka 2007, kulikuwa na visa vya ubakaji pia.

Ni kwa nini makundi mengi yamegeukia mbinu kama hii ya kuwadhulumu wanawake wakati wa mizozo? Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamechukua hatua gani?

Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi amepata kuzungumza na naibu mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu nchini Kenya DR Samwel Tororei. Wasikilize.

(PKG YA JASON NYAKUNDI)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031