Silaha za kemikali hazistahili kuwepo katika karne ya 21:Ban

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameyataka mataifa manane ambayo bado hayajatia saini mkataba dhidi ya silaha za kemikali yajiunge kwenya mkataba huo haraka iwezekanavyo, kwani silaha hizo hazina nafasi katika karne ya 21.

Bwana Ban amesema hayo kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kupinga silaha za kemikali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Amesema ni miaka 15 tangu kuundwa mkataba wa kutokomeza silaha za kemikali, lakini tishio la matumizi ya silaha hizo bado ni kubwa, kwani mataifa hayo manane bado yapo nje ya mkataba. Mataifa hayo ni Syria, Angola, Korea Kaskazini, Misri, Israel, Myanmar, Somalia, na Sudan Kusini.

Nchi 188 zimeutia saini mktaba huo, na thuluthi tatu za silaha za kemikali kote duniani kuharibiwa.

Bwana Ban ameelezea wasiwasi yake kufuatia wawakilishi wa serikali ya Syria kusema kuwa nchi hiyo ina silaha za kemikali na inaweza ikazitumia, na kuitaka serikali ya Syria kuhakikisha usalama wa silaha hizo, akisema matumizi yake litakuwa kosa kubwa na athari zake zitakuwa mbaya mno.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031