Siku ya kupunguza madhara ya majanga duniani, Asia yasaidiwa: IOM

Kusikiliza /

kupunguza majanga

Wakati duniani inaadhimisha siku ya kimatafa ya kupunguza madhara ya majanga duniani, shirika la kimataifa la wahamiaji, IOM limetangaza kuanza kwa mpango mkubwa barani Asia wa kusaidia jamii zilizo hatarini kujiandaa ili kupunguza athari za majanga pindi yanapotokea.

Tayari shirika hilo limepokea dola Milioni 17 kwa kiasi kikubwa kutoka Marekani na Australia ambazo zitatumika kuzijengea uwezo jamii hizo pamoja na serikali na washirika wa kitaifa upunguza madhara ya majanga ambapo ushahidi unaonyesha ongezeko la madhara ya majanga kwa jamii katika muongo mmoja uliopita na kuna uwezekano hali hiyo kuendelea.

IOM inasema wahamiaji wa Asia watapata madhara zaidi kwa kuwa bara la Asia linaongoza duniani kwa kukumbwa na majanga makubwa ya kiasili mara kwa mara na lina idadi kubwa ya wahamiaji hivyo mradi huo ni muhimu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031