Ban atoa rambirambi kufuatia shambulio la kombora nchini Uturuki

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Ahmet Daoud Oglo na kumpa pole kutokana na shambulio la kombora leo alfajiri lililoua watu sita na majeruhi tisa.

Inadaiwa kuwa kombora hilo lilirushwa kutoka Syria na kutua jimbo la Sanliurfa ambapo msemaji wa Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema Bwana Ban ameisihi Uturuki ihakikishe njia zote za mazungumzo na Syria ziko wazi ili kuepusha mgogoro wowote unaoweza kuchochewa na shambulio hilo .

Kwa mujibu wa Msemaji huyo, tayari Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amezungumza na mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa nchi za kiarabu na Umoja wa Mataifa, Lakhdar Brahimi juu ya mgogoro unaoendelea nchini Syria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031