Serikali zapendekeza kupanua orodha ya viumbe walio hatarini ya kuangamizwa

Kusikiliza /

ndovu

Dubu, papa na miti migumu ya Madagascar ni mojawepo wa aina za wanyama kadhaa na mimea ambazo zimepenedekezwa kuongezwa kwenye orodha ya viumbe vinavyolindwa chini ya mktaba wa kimataifa kuhusu biashara katika viumbe walio katika hatari ya kuangamizwa, CITES. Zaidi ya nchi 50 zimewasilisha mapendekezo 67 kwa sekritariati ya CITES, ili sheria zinasodhibiti biashara katika viumbe wa mwituni zifanyiwe marekebisho, ili kuwepo ulinzi na matumizi endelevu ya viumbe hawa.

Katika mapendekezo yao, Burkina Faso, Kenya, Mali na Togo zinatoa wito upigaji marufuku biashara katika pembe za ndovu uongezewe muda. Lakini Tanzania imeomba uwindaji wa ndovu uruhusiwe ndani ya mipaka yake kwa sababu zisizo za kibiashara, ikisema kuwa idadi ya ndovu wake haipo tena hatarini kuangamizwa.

Katibu Mkuu wa mktaba wa CITES, John Scanlon, amesema mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye mkutano ujao wa viumbe wa porini, utakaofanyika mjini Bangkok mwezi Machi 2013.

Hili suala la ndovu wa Afrika na biashara haramu na halali katika pembe za ndovu litakuwa la utata sana. Kilicho dhahiri katika mataifa yote wanachama na mataifa ya Afrika, ni kwamba ni lazima tuchukue hatua za kukomesha uwindaji haramu na biashara haramu katika pembe za ndovu, ambao umeongezeka sasa. Tunaona kuwa kiwango cha mauaji haramu kinapunguza idadi ya ndovu katika maeneo yote barani Afrika.

Katika pendekezo lake, Marekani inataka biashara katika dubu ipigwe marufuku, ikiongeza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa tayari yanamweka mnyama huyo katika hatari ya kuangamia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031