Sera za Italia za kudhibiti mipaka zizingatie haki za binadamu: UM

Kusikiliza /

Francois Crepeau

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wahamiaji Francois Crépeau, amehitimisha ziara yake ya siku tisa huko Italia na kutaka sera za nchi hiyo za kudhibiti wahamiaji haramu zizingatie haki za binadamu.

Ametoa mapendekezo Sita ya kuzingatiwa wakati wa kushughulikia wahamiaji haramu kwenye mipaka ya nje ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, EU ikiwemo makubaliano kati ya Libya na jirani zake yasimlazimishe mhamiaji kurejeshwa katika pwani ya Libya au Italia bila ridhaa yake.

Halikadhalika mashirika ya kimataifa ikiwemo UNHCR na IOM pamoja na wanasheria waruhusiwe kuzungumza na wahamiaji wanapokuwa wamekamatwa au wanashikiliwa na kwamba kuwepo na mfumo utakaowezesha wahamiaji haramu walioko gereza watambuliwe katika kipindi kisichozidi miezi sita.

Wakati wa ziara hiyo nchini Italia ambayo ni sehemu ya ziara za mwaka mzima za kujifunza mifumo ya udhibiti wa mipaka ya nje ya EU, Crepeau alikutana na wawakilishi wa serikali, mashirika ya kiraia na wahamiaji wenyewe na matokeo ya ziara hiyo yatawasilishwa katika kikao cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa mwezi Juni mwakani.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031